Kamisaa wa Sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022, Anne Makinda amewataka viongozi kutumia takwimu katika kupanga na kutekeleza maendeleo ya wananchi.

Makinda ametoa wito huo mkoani Kigoma, wakati alipokuwa akifungua hafla ya usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi.

Anne Makinda.

Amesema, hakuna sababu kwa viongozi kuvutana katika kupanga shughuli za maendeleo kwani kila kitu kinaonekana kwenye takwimu za sensa.

Aidha, Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesisitiza matumizi sahihi ya takwimu wakati wa upangaji huo wa shughuli za maendeleo.

Serikali yatoa mwongozo mahitaji ya chakula wanaokabiliwa na njaa
Serikali yajivunia mafanikio kupitia PEPFAR