Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamsaka Dereva na Utingo wake ambao walikimbia mara baada ya kutokea ajali iliyouwa watu sita wanaosadikika kuwa ni wahamiaji haramu na wengine wanane kujeruhiwa, ambao inasemekana walikuwa wakisafirishwa isivyo halali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP John Makuri amesema kitendo cha kusafirisha mizigo huku wakiwa umeficha raia wa kigeni hakiwezi kukubalika na kwamba wataendelea kufanya na operesheni na msako mkali, Ili kuweza kubaini mtandao wa watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.

Akizungumza katika eneo la Iyayi Wilayani Wanging’ombe Mkoa wa Njombe, amesema ajali hiyo ilitokea majira saa 4:30 usiku, ambapo Lori lenye namba za usajili T.501 AGJ aina Scania likiwa na tela lenye namba T.595 ANG lilipindukia na kusababisha vifo hivyo sita na majeruhi nane kati yao inasemekana kuna raia wa kigeni kutoka nchi ya Ethiopia.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Claudia Kitta amesema tukio hilo ni la kusikitisha kwani watu hao ambao inasadikika walikuwa wanasafirishwa kwenda nchi nyingine, bila kufuata taratibu na Sheria za nchi na miili ya marehemu ilihifadhiwa katika Hospitali ya Ilembula iliyopo wilaya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe.

Zifuatazo ni picha mbalimbali zikionesha matukio tofauti baada ya ajali hiyo.

Mashabiki Young Africans waongeza mzuka Kigali
Maguire awatahadharisha mabeki Man Utd