Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amepongeza uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha vinywaji vikali cha Mati Super Brands Limited, ambacho kimekua mstari wa mbele katika ulipaji kodi kwa Serikali na kujitoa kusaidia jamii inayowazunguka.

Sendiga ametoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Wilayani Babati Mkoani Manyara ambacho pia kimekuwa kikitoa fursa za ajira kwa vijana wa Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga.

Amesema, “sisi kama Serikali tunawapongeza kwa ulipaji mzuri wa kodi za serikali ambao unachangia Maendeleo  kwa taifa kwa ujumla kalini pia mmekua mstari wa mbele kujitolea katika masuala ya kijamii.”

Sendiga ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji, ili waweze kufanya kazi zao bila usumbufu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mati Super Brands Limited, David Mulokozi amepongeza Serikali kwa kuweka mazingira bora kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

Amesema, “kwasasa Serikali imeweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi ambayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara kufanya kaziĀ  na kulipa kodi kwa hiyari.”

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 17, 2023
Wapewa agizo kutatua changamoto za Wafanyabiashara