Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi katika ngazi zote, kuwasikiliza Wananchi na kujielekeza kwenye utatuzi wa kero mbalimbali zinazowakabili.

Rais Samia, ametoa tamko hilo wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Newala
katika uwanja wa Sabasaba, mara baada ya kupokea taarifa za miradi ya maendeleo
Wilayani humo.

Akihutubia wananchi katika uwanja wa Majaliwa Wilayani Tandahimba, Rais Samia pia amewaagiza Madiwani kusimamia vyema fedha za Halmashauri pamoja na fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali, ili waweze kuwahudumia wananchi.

Aidha, Rais Samia pia ametaka viongozi wasimamie vizuri fedha za ruzuku zinazotolewa kwa Wakulima, ili ziweze kuzalisha zaidi na amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kuhakikisha wanasimamia Wakulima kupata pembejeo zinazotolewa na serikali ili kuepuka
utolewaji wa takwimu za uongo.

Rais Samia ameendelea na ziara yake mkoani Mtwara ambapo ameweka Jiwe la msingi jengo la utawala katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na amezungumza na wananchi wa kijiji cha Nanguruwe Wilaya ya Mtwara Vijijini, pamoja na kusalimia wananchi wa kata ya Nanyamba.

Upinzani wafikisha saini Mil. 10 za wanaoipinga Serikali
DC Mtambule aongoza zoezi usafi wa Mazingira