Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Mtwara, wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuimarisha huduma ya Maji Mtwara mjini sambamba na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwa kusimamia vema maelekezo aliyotoa juu ya kuboresha Miundombinu ya Maji Mtwara Mjini.

Hatua hiyo inafuatia Magari yenye shehena ya mabomba ya maji ya mradi mkubwa wa marekebisho ya miundombinu ya maji Mtwara mjini unaogharimu Shilingi 19 Bilioni kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama wakiongozwa na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mtwara Viwanja vya shule ya Msingi Lilungu.

Akizungumza katika tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara – MTUWASA, Mhandisi Rejea Ng’ondya ametoa maelezo kwa Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa, Saidi Nyengedi juu ya ujio wa mabomba ya maji maboresho ya miundombinu ya maji yanayoendelea.

Amesema, dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wa Mtwara wanapata huduma ya maji safi na salama na amedhamiria kumaliza kabisa changamoto ya Miundombinu chakavu Mtwara mjini ikiwa tayari Mradi wa ujenzi wa Chujio la Kusafisha Maji umekamilika na atauzindia yeye mwenyewe wiki ijayo katika ziara yake Mkoani Mtwara.

Ndege Nyuki yauwa zaidi ya 40 Sokoni
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 11, 2023