Mgomo wa Wanachama wa Muungano wa United Auto Workers – UAW, ambao pia ni wafanyakazi wa Makampuni matatu ya kutengeneza Magari Nchini Marekani umefikia siku yake ya tatu bila azimio lolote kutarajiwa.

Takriban wafanyakazi hao 12,700 wa UAW, walishiriki mgomo katika viwanda vitatu, vinavyomilikiwa na Ford, Stellantis, na GM, katika hatua muhimu zaidi ya wafanyakazi wa viwanda nchini Marekani katika miongo kadhaa.

Viongozi wa Makampuni hayo, hawakuonekana kujibu madai hayo ya mkataba mpya, huku watengenezaji magari wakidai nyongeza ya takribani asilimia 20 katika pendekezo la kandarasi ya miaka 4 na miezi sita, ikijumuisha nyongeza ya asilimia 10 ya papo hapo.

Kwamujibu wa Rais wa UAW, Shawn Fain amesema maendeleo ya mazungumzo hayo yamekuwa ya polepole na bado hakuna muafaka ingawa wanatarajia kuwa kila kitu kitaenda sawa na kuondosha sintofahamu iliyojitokeza katika Viwanda hivyo.

TAKUKURU yapewa rungu vyama visivyowalipa Wakulima
Kocha Man Utd arudisha majibu kwa mashabiki