Mwanamuziki Mkongwe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, Damien Aziwa Garcie “Damien Aziwa” kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa kijamii wa Facebook amesema gharama za mazishi ya Mkongwe wa kupiga Rythim Gitaa na Mwanamuziki Lokassa Kasia Denis, maarufu kama Lokassa ya Mbongou zimepanda hadi Dola 10,000.

Bila kufafanua wala kusema nani anatakiwa kulipa gharama hizo, Aziwa amesema gharama hizo tayari zimeoanda ili kumzika mwanamuziki huyo aliyefariki miezi sita iliyopita, ambaye bado hajazikwa jambo ambalo limezua wasiwasi miongoni mwa mashabiki wake Ulimwenguni.

Lokassa alifariki katika Hospitali ya St. Josephs iliyopo Nashua nchini Marekani Machi 14, 2023 akiwa na umri wa miaka 80 baada ya kuugua kwa muda mrefu na mwili wake kurejeshwa Kinshasa mwezi Aprili, ambapo ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Hata hivyo, katika mahojiano ya hivi karibuni na kituo kimoja cha Televisheni, watoto wawili wa Lokassa walitoa wito kwa Serikali ya DRC, kusaidia mipango ya mazishi yake na taarifa kutoka Kinshasa zinasema Wizara ya Utamaduni na Sanaa ingeshiriki kwa kina katika mipango ya mazishi kama ilivyokuwa kwa magwiji wengine wa muziki wa Kongo.

Simon Kjær awaomba radhi The Rossoneri
Ntibazonkiza aweka rekodi mpya CAF