Katibu Mkuu OR-TAMISEMI ametakiwa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi 7 wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi, kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hali iliyopelekea kuzorotesha utendaji kazi na shughuli za Halmashauri hiyo.

Agizo hilo, limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa ambaye pia ametaka hatua hizo za kinidhamu zichukuliwe kwa mujibu wa Kanuni ya 42 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022 inayoainisha kuwashusha vyeo, kukatwa mshahara kwa asilimia 15 kwa muda usiopungua miaka 3 pamoja na kufukuzwa kazi iwapo watabainika kufanya makosa hayo.

Watumishi hao ni pamoja na Kaimu Mhandisi wa Wilaya, Sisty Njau, Mkuu wa Idara ya Maliasili, Damasi Mumwi, Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika, Mustafa Magembe, Mkuu wa Idara ya Ugavi na Ununuzi, Vinsent Moyo na Mkuu wa Idara ya TEHAMA, Mohamedi Songolo.

Wengine ni Katibu wa Afya, Sadick Bakari Khatibu na Afisa Ugavi na Ununuzi, Tunu Mtamaha ambaye alihamishiwa Halmashauri ya Wilaya Kilwa na tayari Waziri Mchengerwa ameelekeza kuanzia sasa Maafisa wote wenye kesi za rushwa na ubadhirifu wasihamishwe vituo vyao vya kazi, mpaka mashauri yao yanapokamilika.

Dkt. Mpango ashiriki ufunguzi Mkutano SDGs New York
Vitabu Vitakatifu navyo vinakataza uhalifu - Insp. Msangi