Jeshi la Urusi limefanya mashambulizi katika eneo la Odessa, kwa ndege 19 zisizo na rubani na makombora mawili yaliyoleta uharibifu mkubwa wa eneo hilo.

Aidha, silaha za Calibers 12 zilizifyatuliwa katika mikoa mbalimbali ya Ukraine huku miundombinu ya Bandari ikiharibiwa kufuatia mashambulizi hayo.

Vikosi vya ulinzi vya Kusini mwa Urusi vilisema katika eneo la Onyxes waliharibu maghala ya nafaka, wakitoa picha zinazoonyesha athari za mashambulio hayo.

Kulingana na mkuu wa utawala wa kijeshi wa mkoa, Oleg Kiper, ghala na nyumba ya kibinafsi katika mkoa wa Odessa pia viliharibiwa.Raia mmoja mwanamke pia alijeruhiwa baada ya kuangukiwa na vifusi vya majengo.

Dkt. Msonde atoa maagizo sekta ya Elimu
Harusi yageuka msiba, mamia wafariki kwa Moto