Takriban Watu sita wameuwawa wakiwemo Watoto na Wanajeshi huku wengine zaidi ya 10 wakijeruhiwa katika mlipuko wa bomu la kutegwa kwenye gari uliotokea katika jimbo la kati la Hirshabelle, lililopo Nchini Somalia.

Akihojiwa na Vyombo vya Habari Meya wa mji huo, Saadaam Cabdi Iidow amesema mtu huyo akiwa kwenye Gari tayari kwa kujitoa muhanga alishaambuliwa na maafisa wa usalama kabla ya kufikia lengo ingawa alifanikiwa kulipua bomu kabla kufikia kizuizi cha polisi.

Amesema, “Mshukiwa wa kutega bomu hilo alilenga kutekeleza shambulio lake kwenye soko la Nyama lenye shughuli nyingi katika mji wa Bulobarde, uliopo takriban kilomita 220 kaskazini mwa Mogadishu na mlipuko huo uliharibu eneo lote la biashara na baadhi ya majengo ya makazi.”

Wakati huo huo, maafisa wa usalama wa Mogadishu wamefanikiwa kuzuia mashambulizi mawili ya mabomu ya kujitoa mhanga kwenye gari, yaliyolenga kushambulia eneo la Dhusamareb, lililopo mji wa umbali wa kilomita 280 kaskazini mwa Mogadishu.

Wimbi la uhamiaji lazidi kuitikisa Dunia - UNHCR
Uhalifu: Wazazi, Walezi wapewa mbinu kuwalinda Watoto