Kuchaguliwa kwa Rais Hassan Sheikh Mohamud kunaweza kushawishi utawala wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), kuipa fursa nchi ya Somalia kujiunga na jumuiya ya umoja huo, pamoja na kuwa taasisi zake bado zinaendelea kuimarishwa.

Jumuiya ya Afrika Mashariki, tayari imeanza kutathmini ustahiki wake wa kujiunga na umoja huo kutokana na hatua hiyo ambayo inafuatia historia ya kukubaliwa kujiunga kwa Sudan kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, zote mbili zikikabiliwa na mzigo mkubwa wa kukabiliana na vita.

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud. Picha ya E-Magazine.

Nchi ya Sudan Kusini, ilikubaliwa rasmi kujiunga mwaka 2016 lakini imeshindwa kufuata kikamilifu itifaki za jumuiya hiyo.

Kwa mara ya kwanza, Somalia iliomba kujiunga na EAC mwaka 2012 lakini ilikataliwa kutokana na misukosuko inayotokana na Al-Shabaab na ukosefu wa sheria thabiti kwa wakati huo.

Geita Gold FC yazipiku Simba SC, Young Africans
Uongozi Simba SC wapata baraka TFF