Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philipo Mulugo amelazimika kujilaza chini kwenye vumbi ili achafuke kama walivyochafuka Wananchi akilenga kuwashukuru kwa mapokezi waliyomuonesha katika ziara yake Kata ya Udinde Wilayani Songwe.

Mulugo ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu amesema amechukua uamuzi huo kama ishara ya shukrani kutokana na wingi wao wa kumpokea huku baadhi yao wakitandika kanga na vitenge chini, ili apite na wengine wakifuta vumbi kwenye viatu vyake na kudai kulala kwake chini anataka kuchafuka kama wao.

Katika ziara hiyo ya kutembelea na kukagua miradi, kuzungumza na Wananchi na Viongozi wa Serikali na Chama, pia Mulugo alitoa kiasi cha Shilingi Milioni 10 za kuviwezesha vikundi 16 vya Wajasiriamali katika Kata hiyo.

Aidha, Mbunge huyo pia amechangia Shilingi milioni tatu kwa ajili ya kununua mashine ya kunakili ya Shule ya Sekondari ya Serikali ya Philipo Mulugo, iliyopo Kata ya Udinde na Shilingi milioni saba za ujenzi wa soko la Mtaa wa Nyerere uliopo Kata ya Udinde, Wilaya na Mkoa wa Songwe.

Bomboka FC wakabidhiwa Bima za Afya
Chuo Kikuu India kumtunuku Rais Samia Shahada ya heshima