Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, Cecilia amesema mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo ambao umefikia asilimia 95, umegharimu shilingi bilioni 3.5 na unatarajiwa kukamilika Machi 31, 2023.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Jengo la Hospitali ya Wilaya, unaohusisha majengo ya huduma za wagonjwa wa nje, mionzi, maabara, wodi tatu za magonjwa mchanganyiko, famasia, utawala, mama na mtoto, huduma ya dharura, upasuaji, uchunguzi, jengo la kuhifadhia maiti na wodi mbili za upasuaji.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea wakati wa ufunguzi wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Songwe.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Songwe, Philipo Mulugo ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuridhia utoaji wa fedha ambazo zinatumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo, ikiwemo ya afya, maji na elimu.

Hata hivyo, mbunge huyo ameiomba Serikali iwajengee barabara ya kutoka Mbalizi-Changombe-Mkwajuni-Saza-Patamela-Makongorosi yenye urefu wa kilomita 118 kwa kwa kiwango cha lami, ili kurahisisha usafiri wa watu na mizigo.

Rais Samia ashuhudia utiaji saini miradi ya Trilioni 1.9
Marufuku kutumikisha watoto machimbo ya Madini: Majaliwa