Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza Wakuu wa Wilaya kwenye maeneo yenye shughuli za uchimbaji wa madini, kuhakikisha wanakemea vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na kuwapeleka shule kwa ajili ya kupata elimu.

Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Songwe inayojengwa katika kata ya Mkwajuni, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema “Kumeibuka tatizo la ukatili wa kuwatumikisha na vitendo vya hovyo wanavyofanyiwa watoto wetu kwenye maeneo hayo fanyeni uchungu na kubaini wanaohusika na vitendo hivyo. Mkuu wa wilaya hakikisha unatokomeza ukatili kwa watoto na wanawake.”

Waziri Mkuu ameongeza kuwa, Viongozi wa machimbo ya madini katika maeneo mbalimbali nchini wafanye uhakiki wa watu wote wanaofanya kazi katika maeneo hayo, na wahakikishe watoto wote walio kwenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa.

Ujenzi Hospitali ya Wilaya wagharimu Bil. 3.5
Familia ya kijana aliyeuawa pamoja na AKA yatoa tamko