Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uchukuzi na Biashara Iringa LTD, Caroline Mwakabungu amemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kumsaidi ili apate hati ya kampuni hiyo, ambayo ilichukuliwa mwaka 2019 na Tume ya uchunguzi wa mali za serikali.

Mwakabungu, alitoa ombi hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu usumbufu pamoja na manyanayaso ambayo wamekuwa wakiyapata kutoka kwa wanasiasa na mamlaka mbalimbali za kiserikali na kuongeza kuwa hati hiyo ilichukuliwa mikononi mwa marehemu baba yake Dkt. Lucas Mwakabungu, aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kwa madai kuwa wanakwenda kuikagua.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uchukuzi na Biashara Iringa LTD, Caroline Mwakabungu.

Amesema, “mwaka 2019 walikuja watu kutoka Tume ya uchunguzi mali za serikali iliyoundwa wakati wa utawala wa hayati Rais Magufuli na kampuni hii kabla ilikuwa mali ya serikali ikijulikana kama RETCO,lakini mzee wangu na wenzake walinunua wakati ule wa sera ya ubinafsishaji chini ya uongozi wa Rais Mkapa.

“Walipokuja wakadai kuwa wao ni tume ya serikali ambayo inakagua mali za serikali kama ziliuzwa kihali baba alijaribu kugoma kutoa hati ile lakini walimwambia kama anakataa watampa kesi ya uhujumu uchumi ikabidi aitoe lakini hadi leo hatujui ipo wapi kwani tumeenda hadi Hazina wanadai hawajui ilipo”ameongeza Mwakabungu.

Ameongeza kuwa, kutokana na hali hiyo hawajui hatma yao na wanashindwa kuingia ubia na wawekezaji wengine au kukopa fedha na hivyo kukosa mtaji wa kujiendesha na kuikosesha mapato serikali.

Familia ya kijana aliyeuawa pamoja na AKA yatoa tamko
Wahusika kifo cha Rais wapandishwa kizimbani