Familia ya Tebello ‘Tibz’ Motsoane, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa pamoja na rapa, Kiernan Forbes maarufu ‘AKA’, mapema Ijumaa ya juma lililopita, iliweka wazi kuwa bado haikuwa imepokea taarifa zozote kutoka kwa polisi kuhusu kifo cha kijana wao.

Familia ya Motsoane, ambaye alikuwa rafiki wa karibu na meneja wa zamani wa AKA, inasema kifo chake cha ghafla kimeacha kovu lisilofutika mioyoni mwa wazazi wake.

Motsoane anaaminika kupigwa risasi kifuani muda mfupi kabla ya yeye na mwanamuziki huyo kukaribia kuachana.

Familia yake, inayoishi Gauteng, iliamua kusafiri kuelekea Durban siku ya Jumapili, ili kupata taarifa zaidi kutoka kwa jeshi la polisi huko Durban.

Mwakilishi wa familia, Ntsoaki Mothakathi, amesema kuwa bado wanajaribu kukubaliana na hali halisi juu ya tukio lililopelekea kifo cha Motsoane.

“Wazazi wamehuzunika baada ya kumpoteza kijana wao, wanapitia nyakati ngumu sana, Kwa sasa familia inapitia mengi, familia imeomba huruma na nafasi inapojiandaa kwa hafla ya mazishi yake.” Amesema Ntsoaki.

Rapa AKA afariki kwa kupigwa risasi

Marufuku kutumikisha watoto machimbo ya Madini: Majaliwa
Mwekezaji amlilia Rais Samia uporaji hati ya kampuni