Mwimbaji nyota wa muziki wa rap nchini Afrika Kusini, Kiernan Jarryd Forbes (35), maarufu kama ‘AKA’ ni mmoja kati ya watu wawili waliouawa wakiwa kwenye gari kwa kupigwa risasi jijini Durban nchini Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani kutumbuiza.

Taarifa za ndani zimeeleza kuwa, wawili hao walipigwa risasi majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika ya kusini Februari 10, 2023 baada ya magari mawili kupita huku watu waliokuwemo ndani wakifyatua risasi wakati AKA na mwenzie wakiwa wamesimama nje ya Mkahawa.

Kiernan Jarryd Forbes (35), ‘AKA’. Picha ya Ladies House.

AKA alikuwa anatarajiwa kutumbuiza katika kilabu cha usiku kiitwacho YUGO lakini hafla hiyo ilighairishwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii ilisema kuwa tamasha hilo lilikuwa likiachwa “kwa sababu ya hali zisizotarajiwa”.

Akisimulia tukio hilo Mhudumu wa afya, Garrith Jamieson alisema, “Walipofika, wahudumu wa afya walikutana na machafuko makubwa na eneo ambalo wanaume wawili, wanaoaminika kuwa na umri wa zaidi ya miaka 30, walipata majeraha mengi ya risasi.

Mzazi mwenzie na AKA, DJ Zinhle akiwa na Binti yake Kairo Olwethu Forbes. Picha na Instagram ya DJ Zinhle.

Alisema, “Wahudumu wa afya waliwasaidia watu hao na kwa bahati mbaya mwanamume wa kwanza alikuwa amepata majeraha mengi ya risasi na hakuonyesha dalili zozote za uhai na alitangazwa kuwa amefariki katika eneo la tukio na huyu AKA alipigwa risasi sita.”

Kiernan Jarryd Forbes, ‘AKA’ alizaliwa Cape Town nchini Afrika Kusini Januari 28, 1988 na alijiingiza katika anga ya muziki mwaka 2002 alipoanzisha kundi la Hip-Hop lililoitwa Entity pamoja na wasanii wenzake, Vice Versa na Greyhound.

AKA na binti yake. Picha yake. Picha ya GH Gossip.

Kutokana na ubora wa mashairi yao, waliteuliwa kuwania Tuzo ya KORA kipengele cha cha Hip-Hop Bora Afrika kabla ya kusambaratika mwaka wa 2006 na baadaye AKA aliendelea kufanya kazi kwa kujitegemea ‘solo artist’ na kutoa kwa albamu yake ya kwanza ‘Alter Ego’ mwaka wa 2011.

Albamu nyingine tatu zilifuata ikiwemo ya siku za karibuni ya 2018 iitwayo ‘Touch My Blood’ na katika maisha yake AKA alikuwa na uhusiano na mtayarishaji wa muziki Ntombezinhle Jiyane, maarufu kama DJ Zinhle mwenye umri wa miaka 39.

Anele Tembe ‘Nelli’ picha ya kushoto na kulia akiwa na Rapa AKA enzi za uhai wao. Picha ya Yomzansi

Walifanikiwa kumpata binti anayeitwa Kairo Olwethu Forbes mwaka 2015 na wenzi hao walitengana mwaka huohuo kabla ya kurudiana tena mwaka 2018 na kutengana tena mwaka 2019 na jambo la kusikitisha ni kwamba AKA alipata mpenzi mpya aitwaye Nelli Tembe, wakachumbiana Februari 2021 lakini Nelli alianguka kwenye kibaraza na kufariki, Aprili 2021.

Wizi ajali ya Korogwe: 14 washikiliwa na Polisi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 11, 2023