Mwanamuzi nyota  wa R&B kutoka nchini Marekani Chris Brown ameshindwa kujizuia baada ya kutopata tuzo ya Grammy katika kipengele kilichomuhusisha, kikizishindanisha album bora za R&B kwa mwaka 2022, ambapo tuzo hiyo imeenda kwa mwimbaji Robert Glasper.

Breezy ameshindwa kujizuia na kuvunja ukimya kutokana na matokeo hayo na kuamua kuutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story) kuweka wazi kotoridhishwa na na suala hilo, ambapo amechapisha picha ya ushindi wa Glasper na kuandika maneno yenye kusomeka “Yalll playing,” akimaanisha ‘mnacheza ninyi’ huku akiambatanisha na emoji za kucheka. “Huyu ni nani?” Aliuliza Breezy.

Mtoto wa Lil Wayne awacharuka wanaomshindanisha baba yake

Katika post hiyo, chris brown ametafsiriwa kama mwenye kuwapiga kijembe Grammy kutokana na kuamini kuwa album yake ilipaswa kuchukua tuzo hiyo na kwamba mwimbaji Glasper hakupaswa kupewa tuzo hiyo kutokana na kutoamini katika uwezo wake na kwamba hata yeye hamjui msanii huyo.

Ujumbe wa Chris Brown kwa waandaaji wa tuzo za Grammy

Glasper ni mpiga piano, mtayarishaji, muandishi na mwimbaji ambaye ameshinda Tuzo hiyo ya Grammy katika kipengele cha Albamu Bora ya R&B kupitia album yake iitwayo ‘Black Radio III’, ambapo alikuwa akichuana na album za wakali wengine kadhaa ikiwamo Breezy ya Chirs Brown (Deluxe), Good Morning Gorgeous ya Mary J. Blige (Deluxe), Candydrip ya Lucky Daye, na Watch the Sun ya PJ Morton.

Katika historia ya muziki, mwimbaji Glasper amefanikiwa kuingia katika vinyang’anyiro vya tuzo za Grammy mara 12, na kufanikiwa kushinda takriban mara tano, Mwaka 2013 aakiwa na albamu bora ya R&B ya Black Radio, Mwaka 2015 Best Traditionali R&B – Performance for Jesus Children, 2017 Best Compilation Soundtrack, 2021 Best R&B Song for “Better Than I Imagined. Best R&B Album 2023.

Kwa upande mwingine mwimbaji Chris Brown yeye amefanikiwa kuingina kwenye vinyang’anyiro takriban 21 na kufanikiwa kushinda mara moja pekee kupitia album yake F.A.M.E mnamo mwaka 2021.

Aliyekuwa mke wa Manara aeleza uhusiano wake na Harmonize

Singida Big Stars yahamishia nguvu Mbeya
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 6, 2023