Jeshi la Polisi Mkoani Tanga, linawashikilia Watuhumiwa 14 wanaodaiwa kuhusika kwenye tukio la wizi katika ajali ya Basi dogo la abiria kugongana na Lori na kusababisha vifo vya Watu 20 Wilayani korogwe Februari 4, 2023 waliokuwa wakisafirisha mwili kwenda Kilimanjaro.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe amesema Wahanga wa tukio walilalamikia kuibiwa baadhi ya vitu vyao ikiwemo vyakula na pesa, ambapo Jeshi la Polisi likafanya uchunguzi na kufanikiwa kuwakamata Watuhumiwa hao.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe.

Amesema, “watu wa kwanza kabisa kushuhudia ajali ni ndugu na ndio watu wa kwanza kuokoa majeruhi, hivyo tutashirikiana nao kwa ukaribu kufahamu vitu mbalimbali vilivyochukuliwa.”

Aidha, amesema katika kudhibiti ajali wameanza ukaguzi maalumu wa magari yote usiku ili kuhakikisha Wananchi wanasafiri salama.

Takwimu: mfumuko wa bei waongezeka
Rapa AKA afariki kwa kupigwa risasi