Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Ihapa Kata ya Old Shinyanga Luhende Heke (80), anayetuhumiwa kumbaka mjukuu wake wa darasa la kwanza (8), anayesoma Shule ya Msingi Old Shinyanga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amesema tukio hilo majira ya saa 4.30 asubuhi na kwamba mtuhumiwa alikamatwa na upelelezi unaendelea.

Diwani wa Viti Maalumu, Picca Chogelo alisema alipata taarifa majira ya saa 7:00 mchana ambapo walimpeleka mtoto huyo kwenye zahanati na daktari akathibitisha amebakwa na kuharibika vibaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi

Naye bibi wa mtoto huyo, alisema hakuwepo nyumbani alikuwa shambani lakini aliporejea alimkuta mjukuu wake analia huku damu nyingi zikivuja sehemu za siri.

“Nilipomhoji mtoto aliniambia amechomwa na mti lakini nikaendelea kumpeleleza akasema amebakwa ndipo nikaenda kwa mwalimu wakati huo baba yake hakuwepo nyumbani,” alisema bibi huyo.

Maelfu wajitokeza kuasili kichanga kilicho okolewa kwenye kifusi
Habari Picha: Uapisho wa Makamishna, Skauti Mkuu