Idadi ya vifo vilivyotokea kutokana na tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria imefikia watu 20,000 huku waokoaji wakifanikiwa kuwapata manusura wengine kutoka kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

Usiku wa kuamkia leo (Februari 10, 2023), waokoaji walifanikiwa kumpata binti mwenye umri wa miaka 10 katika Wilaya ya Antakya ikiwa siku tatu tangu na watu wengine kadhaa pia wamepatikana wakiwa hai katika majimbo ya Adiyaman na Kahramanmaras.

Waokoaji wakitimiza majukumu yao ya kuwatafuta manusura wa ajali ya Tetemeko la ardhi. Picha ya AFP.

Hata hivyo, vikosi vya uokozi vimesema matumaini ya kuwapata watu wengine zaidi wakiwa hai yanapungua kutokana na ukubwa wa vifusi na hali ya hewa kuwa ya baridi sana ingawa bado hawajakata tamaa.

Vifo hivyo, vilivyosababishwa na tetemeko hilo la ardhi ambalo linatajwa kuwa baya zaidi katika kipindi cha muongo mmoja, vikipindukia idadi ya wale waliopoteza maisha katika tetemeko lililoipiga nchi ya Japan mwaka 2011.

Aboutwalib Mshery mambo safi Tunisia
Azam FC kunoa makali kwa KMKM