Hatimaye Mlinda Lango chaguo la Pili wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Aboutwalib Mshery amefanyiwa upasuaji ‘Operesheni’ Mjini Sousse nchini Tunisia.

Mlinda Lango huyo aliongozana na Kikosi cha Young Afrika hadi nchini humo, kwa ajili ya kufanyiwa matibabu ya majereha ya mguu, ambayo yamemuweka nje kwa muda mrefu.

Aboutwalib Msheri baada ya kufanyiwa upasuaji ‘Operesheni’ Mjini Sousse nchini Tunisia.

Taarifa ya Daktari iliyowekwa katika ukurasa rasmi wa Young Africans ilieleza kuwa Operesheni ya Mlinda Lango huyo kinda imefanyika salama na Jumamosi Mshery anatarajia kurudi Jiji la Tunis kuungana na timu hiyo.

“GOLIKIPA wetu Mshery amefanyiwa operesheni leo mjini Sousse hapa Tunisia.

Wananchi tunakuombea upone na kurudi uwanjani haraka??” imeeleza taarifa ya Young Africans iliyochapishwa kwenye kurasa za Mitandao ya Kijamii za Klabu ya Young Africans.

Singida Big Stars yakubali yaishe Ligi Kuu
Tetemeko Syria, Uturuki: Vifo vyafikia 20,000