Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Skauti Mkuu, Rashid Kassim Mchatta katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma hii leo Februari 10, 2023.

Mara baada ya uapisho huo, Rais Samia alifanya pia mazungumzo na Viongozi mbalimbali na yafuatayo ni baadhi ya matukio katika picha wakati wa uapisho huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Viongozi mbalimbali mara baada ya hafla ya Uapisho wa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Skauti Mkuu Rashid Kassim Mchatta katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Februari 10, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Mawaziri, Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Skauti Mkuu Rashid Kassim Mchatta wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Februari 10, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Rashid Kassim Mchatta kuwa Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, Februari 10, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dosca Kemilembe Mutabuzi kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, Februari 10, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bahame Tom Mukirya Nyanduga kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, Februari 10, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Gerald Mbonimpa Ndika kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, Februari 10, 2023.

Mzee wa miaka 80 mbaroni kwa kumbaka mjuu wake
Ihefu FC yaitangazia vita Singida Big Stars