Wafuasi wa Kiongozi wa zamani wa waasi, Fr̩d̩ric Bintsamou maarufu kama Mchungaji Ntumi, wameiomba Serikali ya Kongo ya Brazzaville, kutoa nafasi rasmi kwa kiongozi wao, kama ambavyo walikubaliana juu ya kulimaliza mzozo wa kivita ambao ulitikisa eneo la Pool, kusini mwa nchi hiyo mwaka 2016 Р2017.

Kiongozi anayesimamia chama cha upinzani cha CNR kinachoongozwa na Mchungaji Ntumi, Bi. Ané Philippe amesema wameamua kuiomba Serikali kutokana na ukimya wa zaidi ya miaka mitano baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, huku kukiwa hakuna ishara ya kuamua hadhi ya Kiongozi wao.

Amesema, “Kiongozi wetu lazima awe wa kwanza kupewa nafasi muhimu au kupewa hadhi kubwa hadhi yake lazima ibainishwe, sanjari na kuwarejesha wapiganaji wa zamani katika maisha ya kiraia au kuingizwa katika vikosi vya usalama na ulinzi.”

Mchungaji Frédéric Bintsamou almaarufu “Ntumi”. Picha ya AFP.

Mchungaji Ntumi na wapiganaji wake wa zamani wa ‘ninja’ ambao walishiriki katika mzozo wa awali wa Pool mwaka 1998 – 2003 waliopinga kuchaguliwa tena kwa Rais Denis Sassou Nguesso 2016, walichukua silaha dhidi ya utawala wa Brazzaville.

Makubaliano ambayo yalimaliza mgogoro huo mwishoni mwa mwaka 2017 yalitoa, pamoja na mambo mengine, kwa ufafanuzi wa hadhi maalum ya Bw. Ntumi, kupokonywa silaha na kuingizwa katika vijkosi vya usalama na ulinzi kwa wapiganaji wa zamani ili ‘kuimarisha amani’.

Tangu wakati huo, Ntumi amekuwa akiishi katika ngome yake ya Pool, eneo lenye rutuba kwa muda mrefu ambalo lilizingatiwa kuwa kikapu cha mkate cha Brazzaville, wakati serikali inadai kukusanya na kuharibu angalau silaha 8,000.

NIC watoa elimu huduma za Kidijitali
Umeme ni janga la Kitaifa: Rais