Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa (70), ametangaza janga la kitaifa katika jaribio la kukomesha tatizo kubwa la umeme, ambalo linadhoofisha maisha na uchumi wa nchi hiyo yenye ustawi wa viwanda barani Afrika.

Kupitia hotuba yake ya kila mwaka kupitia Luninga nchini humo, Ramaphosa amesema, kwa miezi kadhaa, Waafrika Kusini milioni 60 wamelazimika kupika, kufua nguo na kuchaji simu zao nyakati fulani za mchana pekee.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa (70). Picha ya IOL.

Amesema, “tunatangaza janga la kitaifa ili kukabiliana na tatizo la umeme na athari zake mara moja na katika hali ya kukipekee, hatua za haraka zitachukuliwa kwa sasa, kazi kubwa ni kupunguza mgao unaoendelea, ili kukomesha na kuondokana kabisa na hali hiyo.”

Kwa upande wake Chama tawala cha African National Congress – ANC, katika wiki iliyopita kilisema kimetoa maelekezo ya wazi na kuitaka serikali kuhakikisha maeneo ya Hospitali na mitambo ya kusafisha maji taka isipewe mgao wa umeme.

Bibi aitaka Serikali kumtambua Ninja wa Pool
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 10, 2023