Ihefu FC imeapa kulipa kisasi kwa Singida Big Stars, kuelekea mchezo wa Mzunguuko wa 23 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa keshokutwa Jumapili (Februari 12).

Ihefu FC itakua nyumbani Highland Estate kuikabili Singida Big Stars kwa mara ya kwanza tangu ilipopanda Daraja na Kucheza Ligi Kuu msimu huu 2022/23.

Afisa Habari wa Klabu hiyo yenye maskani yake Wilayani Mbarali mkoani Mbeya Peter Andrew amesema, wamehamiria kucheza kwa kujiamini keshokutwa, huku wakihakikisha lengo la kulipa kisasi linatimizwa ndani ya dakika 90.

Amesema wanaifahamu vizuri Singida Big Stars, kwani walicheza nayo msimu uliopita walipokua Ligi Daraja la Kwanza ‘Championship’, lakini keshokutwa itakuwa mara yao ya kwanza kukutana na miamba hiyo ya Singida Uwanja wa Highland Estate katika mchezo wa Ligi Kuu.

“Tunaifahamu vizuri Singida Big Stars tangu tupo Ligi Daraja la Kwanza ‘Championship’ kipindi hiko ikiitwa DTB, lakini hayo mambo yashapita, sasa hivi tupo Ligi Kuu na tupo tayari kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wa Duru la Kwanza katika Uwanja wao wa nyumbani” amesema Peter Andrew

Ikumbukwe kuwa Oktoba 24-2022, Ihefu FC ilipoteza dhidi ya Singida Big Stars katika Uwanja wa Liti mjini SIngida kwa kufungwa 1-0.

Habari Picha: Uapisho wa Makamishna, Skauti Mkuu
Mtibwa Sugar yatamba Ligi Kuu