Aliyekuwa Kiongozi wa Extra Musica (Original), Ibambi Okombi Rogatien maarufu kama Rogaroga ambaye kwasasa analiongoza kundi la Extra Musica lililomeguka, , amezusha mjadala mtandaoni baada ya kuchapisha taarifa za kuomba mtu yeyote mwenye nyimbo za video za kundi hilo aziwasilishe na atapatiwa zawadi.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Rogaroga ameandika kwa kuanza na salam kisha kuweka ujumbe huo akitaka nyimbo hizo kisha kuweka mawasiliano na hivyo kufanya wadau wa muziki kuhoji iweje kundi hilo kubwa barani Afrika na ulimwenguni kiujumla likose maktaba ya nyimbo zake.

Wadau hao wamesema bendi hiyo ni kongwe na kuandika ujumbe huo mtandaoni ni kuonesha udhaifu na kujishusha thamani kwa wakongwe hao waliopata kutamba katika ulimwengu wa muziki Barani Afrika na ulimwenguni kote kwa mashabiki wa mtindo wa soukous.

#

Extra Musica, ni bendi kuu ya muziki kutoka katikati ya Kongo Brazzaville na lilianzishwa katikati ya miaka ya 1990 kwa kutengeneza muziki wao kisasa na wakitumia kucheza mtindo wa soukous ambapo albamu zao za kwanza ndizo zilizofanikiwa zaidi si tu katika nchi yao bali kote Barani Afrika.

Chini ya uongozi wa mpiga ngoma, Ramatoulaye na mpiga gitaa Roga Roga, Extra Musica imekuwa na mafanikio kwa miaka mingi na kutoa albamu kadhaa ambapo baadaye kundi hili lilikubwa na matatizo ya hali ya kifedha na kukosa usimamizi thabiti na hivyo kuanza kuporomoka na kuleta migawanyiko.

Baada ya kuondoka kwa Guy Guy Fall, mwaka 1996, wengine waliondoka mwaka 1998 na kuunda kundi kisha kutengeneza vibao moto wakijiita Extra Musica International chini ya uongozi wa Quentin Mouyasko, akiwa na mpiga gitaa Arnaud Laguna, Pinochet Thierry, Durell Loemba na Cyrille Malonga ikiwa ni mwaka 1998.

Ibambi Okombi Rogatien maarufu kama Rogaroga.

Kundi la awali chini ya uongozi wa Roga lilibadilisha jina lake ndani ya Muziki wa ziada na kujiita Extra Musica Zangul ikiwa ni ghani iliyotumika katika album ya Etat Major na kunakshiwa na Atalaku machachari Mazikou Ghislain (Kila Mbongo), na kisha baadaye kutoa albamu ya 2001 « Trop c’est trop » iliyofuatiwa na ukimya mrefu lakini albamu mpya Obligatoire ikaondosha hali hiyo mwaka 2004.

Baadaye mwaka huo (2004), Elenga Laka Bienvenu Dominique (Doudou Copa), aliamua kuondoka na kuanza kufanya kazi peke yake, kisha mwaka 2005, mwimbaji Mbon Sylvain (Oxygène) naye akalikacha kundi hilo la Extra Musica na kuunda bendi yake ya Universal Zangul.

Mgawanyiko wa kundi hili kwa mara ya mwisho umetokea mwaka 2019 baada ya kujitenga kutoka kundi la Mkongwe Rogaroga baada ya kudaiwa kuhitilafiana kwa sababu za kimaslahi.

Afisa Al Hilal aitamani Young Africans
Kocha US Monastir atuma salam Young Africans