Mtunzi na mwimbaji wa wimbo “Mchumba” Msanii wa Bongo Fleva, Hamis Juma Mbizo (H-Mbizo), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Januari 28, 2023.

H-Mbizo amefariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitalini Mkoani Morogoro alipokuwa amelazwa kwa wiki mbili akisumbuliwa na maradhi ya mgongo.

Hamis Juma Mbizo (H-Mbizo), katika picha tofauti enzi za uhai wake.

Baba mzazi wa H-Mbizo, Juma Mbizo akizungumzia kifo cha mwanawe amesema taratibu za kuurejesha mwili wa marehemu kuja Dar es Salaam zinaendelea na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho Jumapili (Januari 29, 2023), saa saba mchana katika makaburi ya Magomeni Ndungumbi.

H-Mbizo alikuwa akisumbuliwa na mgongo na alienda Mkoani Morogoro kwa dada yake kwa mapumziko, lakini baadae alizidiwa na kulazwa Hospitalini na msiba utakuwa nyumbani kwao Magomeni Makanya.

Mamadou Doumbia kuivaa Rhino Rangers
Ukomo magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni 2030