Rais wa Eritrea, Isaias Afwerki ameishutumu Serikali na nchi ya Marekani kwa kuwaunga mkono waasi wa Tigrayan, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika hivi karibuni, kaskazini mwa Ethiopia.

Afwerki ameyasema hayo wakati wa mahojiano na Vyombo vya Habari vya ndani, ambapo alidai kuwa mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya Ethiopia na chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF), uliharakishwa na Marekani ili kuwazuia waasi kushindwa katika uwanja wa vita.

Rais wa Eritrea, Isaias Afwerki. Picha ya News 24.

Katika mahojiano hayo, Afwerki pia alikiri kwa mara ya kwanza kuwa maelfu ya watu walikufa katika mzozo huo, ingawa hakufafanua zaidi juu ya majeruhi wa Eritrea huku akikanusha ripoti ya wanajeshi wa Eritrea kufanya uhalifu wa kivita katika nchi jirani ya Ethiopia.

Jeshi la Eritrea, liliunga mkono vikosi vya Ethiopia wakati wa vita dhidi ya TPLF na limeshutumiwa na Marekani na makundi ya haki za binadamu kwa baadhi ya ukatili mbaya zaidi wa mgogoro huo.

Mwandishi wa Habari atupwa jela kwa tishio la usalama
Wizara yatangaza uwepo homa ya ya kuvuja damu, tisa wafariki