Watu tisa wamefariki kutokana na ugonjwa wa virusi vya Marburg (homa ya kuvuja damu ambayo inakaribia kuua kama Ebola), mashariki mwa nchi ya Guinea ya Ikweta nchi ndogo ya Afrika ya kati ambayo imeweka karantini jimbo moja kwa ajili ya kudhibiti janga hilo.

Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Mitoha Ondo’o amesema Serikali ilichunguza washukiwa wa homa ya hemorrhagi na kuwapata watu watatu pekee walio na dalili ndogo za ugonjwa huo, na kwa sasa wametengwa kwenye eneo la vijijini lenye wakazi wachache linalopakana na Gabon na Cameroon.

Virusi vya Marburg, huambukizwa kwa binadamu na popo. Picha ya PTN.

Amesema, “Guinea ya Ikweta, inatangaza tahadhari ya afya ya homa ya kuvuja damu ya Marburg katika jimbo la Kie-Ntem na katika wilaya jirani ya Mongomo na mpango wa kukinga umewekwa kwa ushirikiano na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO).”

Virusi vya Marburg, huambukizwa kwa binadamu na popo wa matunda na huenezwa kwa binadamu kwa kugusana moja kwa moja na maji maji ya mwili kutoka katika watu walioambukizwa, au kwa nyuso na nyenzo.

Marekani yashutumiwa kuwaunga mkono waasi Ethiopia
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 14, 2023