Video inayosambaa mitandaoni ya Mtu mmoja raia wa Nigeria, Maazi Chukwudiaso Onyema akimtaka mwanzilishi wa Kanisa la Dunamis International Gospel Centre, Dkt. Paul Enenche amrudishie zaka zake kwani ameghairisha kwenda mbinguni na badala yake ataenda kuzimu, imezua taharuki.

Akiwa ameshikilia kadi yake ya fungu la kumi kwenye video hiyo, mwanamume huyo Chukwudiaso Onyema, amesema hakuwa na akili timamu wakati alipokuwa akitoa zaka kanisa na kwamba kwasasa anachofikiria ni kupata pesa zake zote.

Maazi Chukwudiaso Onyema (kushoto) na Mwanzilishi wa Kanisa la Dunamis International Gospel Centre, Dkt. Paul Enenche.

Amesema, ana njaa na kwamba kuna mateso mengi kwani benki yake ilimfelisha kutokana na hali ilivyo nchini Nigeria kwa sasa na kwamba utafiti wake unakuonesha hatafika mbinguni hivyo ni bora akafanyia kazi nyingine fedha hizo.

Onyema ameongeza kuwa, amehesabu pesa zote alizotoa kwenye fungu lake la kumi na anataka zirudishwe kwani toka ajiunge na kanisa la Dunamis mwaka wa 2008, aliambiwa ajiwekee hazina mbinguni kupitia zaka na sasa akiangalia hali ilivyo, anadhani atakwenda kuzimu badala ya kwenda mbinguni kama alivyopanga awali.

Rais amuhamisha Waziri, amtaka akapambane na majambazi
Leo ni siku ya Redio Duniani