2023, ni mwaka wenye shughuli nyingi za kisiasa za bara la Afrika na mwanga wa Demokrasia, kwa nchi nyingi kufanya chaguzi zenye viwango vya juu na vya kutafakarisha, kutokana na mivutano ya kisiasa na hali mbaya ya kichumi kwa karibu mataifa mengi.

Nigeria:

Uchaguzi mkuu wa mwezi Februari nchini Nigeria umeibua matarajio makubwa miongoni mwa wapiga kura vijana, ambao wana hamu ya kuona mwisho wa utawala wa Rais, Muhammadu Buhari.

Huku nchi hiyo ikikabiliwa na mdororo wa kiuchumi na kukithiri kwa ukosefu wa usalama, Wanigeria wanatumai kuwa zoezi hilo linaweza kuleta viongozi wenye nguvu za kukabiliana na kuzorota kwa nchi yao.

Muhammadu Buhari. Picha ya BBC.

Aliyekuwa Gavana wa Jimbo la Lagos Bola Tinubu, Atiku Abubakar wa chama cha People’s Democratic Party na Peter Obi ndio wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumrithi Buhari.

Nchini Sierra Leone – Mwezi Juni, watafanya uchaguzi wa rais na wabunge. Rais Julius Maada Bio anatarajiwa kuwania muhula wa pili.

Chama chake cha Sierra Leone People’s Party, kitakuwa na matumaini ya kuhifadhi wingi wake katika bunge la kitaifa, ambalo limekuwa likitishiwa na kuongezeka kwa gharama za maisha.

Emmerson Mnangagwa. Picha ya Vatican News.

Zimbabwe:

Nchini Zimbabwe, Rais Emmerson Mnangagwa atakuwa na matumaini ya kushinda changamoto mpya ya kiongozi wa upinzani, Nelson Chamisa ambaye chama chake cha Citizens Coalition for Change kimejaribu kuchokoza upinzani na kurekebisha makosa ya 2018.

Wakiwa madarakani tangu uhuru wa Zimbabwe, chama cha ZANU-PF kitakuwa na matumaini ya kuendeleza utawala wake, katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

George Weah. Picha ya The Africa Report.com

Liberia:

Jamuhuri kongwe zaidi barani Afrika, nchi hii inatazamiwa kupiga kura za urais na wabunge mwezi Oktoba 2023 katika kile ambacho kitakuwa hatua muhimu kwa nchi ambayo bado inapata nafuu kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mingi na janga baya.

Rais wa nchi hiyo, George Weah amekabiliwa na shutuma kwa kushindwa kukabiliana na ufisadi uliokithiri na kwa kuwa mbali na nchi yake akitazama Kombe la Dunia nchini Qatar, huku nchi hiyo ikikabiliwa na mdororo wa kiuchumi.

Ali Bongo. Picha ya EURACTIVE.com

Gabon:

Rais Ali Bongo anatarajiwa kuchaguliwa tena nchini Gabon baada ya kupitishwa kimyakimya na wanachama wa chama chake cha Democratic Party.

Licha ya kuugua kiharusi ambacho kilimfanya ahangaike kutembea, chama tawala kinaonekana kutotaka kustaafu kiongozi wake mwenye umri wa miaka 63.

Familia ya Bongo imetawala Gabon yenye utajiri wa mafuta tangu 1967.

Felix Tshisekedi. Picha ya SADC.

DR Congo:

Mwezi Desemba, 2023 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo itafanya uchaguzi mkuu wa kuchagua rais mpya, bunge la kitaifa na seneti na akiwa madarakani tangu 2019, Rais Felix Tshisekedi anatarajiwa kuwania muhula wa pili.

Baada ya kutofautiana na mtangulizi wake ambaye uungwaji mkono wake ulimhakikishia urais, Tshisekedi atalazimika kutafuta washirika wapya kukabiliana na upinzani ambao umekuwa ukifanya maandalizi yake kwa muda mrefu.

Mfanyabiashara maarufu na Gavana wa jimbo la Katanga, Moise Katumbi tayari ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo ya Urais.

Huku mashariki mwa nchi hiyo kukiwa na mzozo, Tshisekedi anaweza kutatizika kuwashawishi Wakongo kuwa yeye ndiye badiliko wanalotaka.

GGML wajivunia Nyankumbu Sekondari kung'ara kidato cha nne
Usalama: Puto la tatu latunguliwa, tahadhari yatolewa