Mwanamke mmoja Rosette Najuma (59), amefariki dunia wakati wakati akifanyiwa maombi katika Kanisa la Christian Life lililopo jijini Kampala nchini Uganda.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Msemaji Msaidizi wa Polisi wa Kampala, Luke Owoyesigyire amesema Najuma alizirai na kufariki wakati ibada ikiendelea katika kanisa hilo eneo la Makerere.

Waumini wakitoka Kanisani baada ya ibada ya Jumapili katika kijiji karibu na eneo la Bauchi nchini, Nigeria. Picha ya World Watch Monitor.

Inadaiwa kuwa, Mwanamke huyo alikuwa akiugua kwa muda wa miaka mitatu na licha ya kufanyiwa vipimo na Daktari hakukutwa na ugonjwa wowote na ndipo aliamua kwenda kanisani kwa ajili ya kuombewa.

Owoyesigyire amesema, rafiki zake waliamua kumtafutia msaada wa kiimani na ndipo walimpeleka katika kanisani hapo ambapo umauti ulimkuta na Polisi bado inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 11, 2023
Dkt. Mollel: Bima ya Afya ni suluhu changamoto ya magonjwa