Serikali nchini, imesema Bima ya Afya kwa wote ndio suluhu ya changamoto za magonjwa yote, kwani wananchi watatibiwa ikiwemo ugonjwa wa Selimundu bila gharama kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali ya taifa.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge Joseph Kakunda katika mkutano wa kumi kikao cha tisa, Bungeni jijini Dodoma hii leo Februari 10, 2023.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel.

Amesema, licha ya Wizara ya Afya kuwahamasisha wananchi kujiunga katika mfuko wa bima ya afya, Serikali imeendelea kutoa fedha, kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya matibabu ya magonjwa hayo.

Aidha, Dkt. Mollel amesema tayari shilingi 11.5 Bilioni zimetolewa na Dkt. Samia kwa ajili ya ununuzi wa kifaa chenye uwezo wa kupima vinasaba, ili kutambua tatizo na kulitibu.

Mama afariki akifanyiwa maombi Kanisani
Serikali yatoa tamko gesi sababishi tabaka la ozoni: Mhandisi