Shirika la Waandishi wa Habari wasio na mipaka – RSF, limeukosoa mchakato wa kisheria kuhusu kifo cha Mwanahabari John Williams Ntwali wa nchini Rwanda.

Ntwali, aliyekuwa Mhariri wa gazeti la The Chronicles na mkosoaji wa Rais Paul Kagame, alifariki Januari 18, 2023 baada ya Pikipiki aliyokuwa amepandwa kugongwa na gari karibu na mji mkuu wa Kigali.

Marehemu, John Williams Ntwali. Picha ya IPI.

Dereva aliyehusika katika ajali hiyo, alikiri kosa na alipatikana na hatia ya kuua bila kukusudia ambapo Februari 7, 2023 alitakiwa kulipa faini ya sarafu milioni moja za Rwanda, ambayo ni sawa na euro 860.

RSF inasema, tangu mwaka 1996 Waandishi wa Habari wanane wameuawa au kupotea nchini Rwanda, huku wengine 35 wakilazimika kwenda uhamishoni huku uhuru wa vyombo vya Habari ukipungua.

Watakiwa kuungana huduma bora za afya ngazi ya jamii
Valentine Day: KONKI tano za kumshangaza umpendae