SERIKALI imepiga marufuku vitabu 16 kutumika mashuleni kutokana na vitabu hivyo kukinzana na mila, desturi na tamaduni za kitanzania .

Aidha imesema, kwa shule ambayo itabainika kuendelea kutumia vitabu hivyo mara baada ya katazo la Serikali itachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kufutiwa usajili wake.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kufutwa kwa vitabu hivyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema uwepo wa vitabu hivyo pia unahatarisha malezi bora ya watoto.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.

Amevitaja vitabu vilivyopigwa marufuku kutumika mashuleni kuwa ni pamoja na Diary of Wimpy Kid, Dairy of Wimpy Kid-Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid- The last Straw, Diary ofi Wimpy Kid –The Ugly Truth na Diary of Wimpy Kid-Cabn Fever.

Vitabu vingine ni Diary of Wimpy Kid –The Third Wheel, Diary of Wimpy Kid –Hard Luck, Diary of Wimpy Kid-The long Haul, Diary of Wimpy Kid –Old School, Diary of Wimpy Kid-Double Down na Diary of Wimpy Kid-The Gateway.

Kwa mujibu wa Profesa Mkenda, pia vitabu vya Diary of Wimpy Kid-Diper Overlode Is for TANSGENDER (you know best who you are), Is for LGBTQIA (find the word that make you na Sex Education a guid to life, vyote havifai na vimepigwa marufuku.

“Hii ni orodha ya kwanza ,baada ya ukaguzi na kuhakikiwa kwamba vitabu hivi vinakiuka maudhui ya malezi mema ya mtanzania,ukaguzi unaendelea ,tunahimiza wazazi ,walimu ,wanafunzi na jamii kwa ujumla kwa ambaye atagundua kitabu kingine chochote kinachokiuka maudhui apige simu kwenye namba 0262160270 au 0737962965, ”amesema Profesa Mkenda.

Waziri huyo, pia ametumia nafsi hiyo kuwahimiza wazazi kukagua mabegi ya watoto mara kwa mara, ili kuhakikisha hawatumii vitabu hivyo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 14, 2023
Serikali kuweka mazingira wezeshi sekta ya utalii