Mamlaka za Usalama nchini Chad, zitaanza kuwasikiliza waasi 150 wanaotuhumiwa kusababisha kifo cha Rais Idriss Déby, katika Gereza la Kléssoum, lenye ulinzi mkali, ambao wanashtakiwa kwa ugaidi, kuandikisha watoto askari, utumwa, kudhoofisha usalama wa serikali, na mauaji ya rais.

Washukiwa hao ni kutoka chama cha Front for Concord and Change in Chad (FACT), lenye vuguvugu la waasi ambalo lilianzisha mashambulizi ya kuipindua serikali ya Chad kutoka kambi zake za nyuma nchini Libya mwaka 2021.

Aliyekuwa Rais wa Chad, Hayati Idriss Déby. Picha ya Daily Sabah.

Idriss Deby, aliuawa kwenye mstari wa mbele mwezi Aprili 2021 wakati akisimamia operesheni za jeshi kuwarudisha nyuma waasi na alikuwa ametoka kushinda mamlaka mpya katika kura iliyoshutumiwa kuwa ya ulaghai.

Kwa msaada wa Ufaransa, watawala wapya wa kijeshi wa Chad waliweza kuwazuia waasi kusonga mbele, na takriban miaka miwili tangu kifo cha Deby, mazungumzo kati ya vuguvugu la waasi na serikali ya Chad yamekwama wakitaka wanachama wake waachiliwe huru.

Mwekezaji amlilia Rais Samia uporaji hati ya kampuni
Hiki ndio chanzo cha bifu la Rihanna na Trump