Mwimbaji Rihanna ndio nyota wa mchezo aliyeipamba Super bowl LVII jumapili usiku, huko nchini Marekani, ambapo onyesho lake lilionyesha kukonga nyoyo za maelfu ya mashabiki zake ulimwenguni kote kasoro aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Ambaye mara kadhaa ameonekana kutumia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kumrushia vijembe mwimbaji huyo.

Punde baada ya onyesho la Rihanna kwenye Super bowl Trump aliandika kuwa onyesho la Rihanna lilishindwa yaani ni sawa na kuwa mwimbaji huyo amefeli.

“Onyesho baya zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya Super bowl” aliandika Trump.

Siku mbili kabla ya mchezo huo, Trump pia alisema

“Bila ‘Stylist’ wake asingekuwa kitu. Kila kitu kibaya, na hana kipaji!”

Rihanna akitumbuiza wakati wa mapumziko ya Super Bowl. Photo BY KEVIN MAZUR/GETTY IMAGES

Wengi wanajiuliza ni kipi chanzo cha vita hii ya maneno kati ya Donald Trump na mwimbaji Rihanna?.

Vita ya wawili hao ilianza wakati ambao Trump alikuwa rais wa taifa la Marekani, tabia za Trump na namna alivyodhihirisha kuwagawa watu ilikuwa moja ya vyanzo vilivyopelekea Rihanna kumchukia Trump.

Hasa wakati ambao Trump alipoanzisha kile kilichojulikana kama ‘marufuku ya Waislamu nchini Marekani’, jambo hili halikumfurahisha Riri na kuamua kuutumia ukurasa wake wa twitter kupinga vitendo vya Trump.

“Nimechukizwa! Amerika inaharibiwa mbele ya macho yetu! Unakuwa nguruwe mpotovu kiasi gani kutekeleza BS kama hiyo!”

Iko wazi kwamba mwimbaji huyo hakumpenda Trump au maamuzi yake wakati akiwa ofisini.

Pia mara kadhaa Rihanna alikuwa akimzungumzia Trump kuhusu tabia zake alizodai kuwa ni mbaya na hata kufikia hatua ya kumzuia kucheza nyimbo zake zozote kwenye mikutano yake ya kisiasa.

Bifu hilo la zito baina ya wawili hao, baada ya kipindi kirefu kupita limerudishwa kwa nguvu wakati wa kipindi cha mapumziko cha Super Bowl.

Rihanna na Donald Trump. photo by Getty Images

Trump amekuwa akionyesha wazi kuwachukia watu wote waliokuwa wakimpinga na Riri yuko kwenye kundi hilo kama mmoja wa watu walioudharau zaidi urais wake.

Trump pia hajawahi kuwa na haya kuwataja watu na kuwatusi, hasa kwenye mitandao ya kijamii, hivyo haikushangaza kwa yeye kutumia mtandao kuwafahamisha wafuasi wake jinsi ambavyo hakupendezwa na chaguo la NFL la msanii Rihanna kutumbuiza kwenye Super Bowl.

Mwanasiasa mwingine wa kihafidhina, mwakilishi wa Texas Jonny Jackson, alisema

“Kwa nini NFL inaonyesha upuuzi huu? Rihanna hapaswi kuwa mtumbizaji wa halftime!!”.

Kitendo cha Riri kutokufumba macho suala maoni yake ya kisiasa, hasa kwa rais wa zamani, ndio jambo pekee lililochochea bifu zito baina ya wawili hao.

Rapa AKA afariki kwa kupigwa risasi

Wahusika kifo cha Rais wapandishwa kizimbani
Mwandishi wa Habari atupwa jela kwa tishio la usalama