Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema katika  Jimbo la Singida Kaskazini  Vijiji 6 vimesalia kuunganishwa na umeme kati ya vijiji 84 vya jimbo hilo.

Kapinga ameyasema hayo wakati akisalimia wananchi  katika Kijiji  cha Sagara,  wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Singida iliyoanza leo Oktoba 15, 2023.

Amesema Vijiji vyote nchini ambavyo havina umeme vitapata umeme kupitia miradi mbalimbali  ya usambazaji umeme vijijini, inayoendelea ukiwemo mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko pili.

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeendelea kuhakikisha Vijiji vyote vinavyotakiwa kuwa na Umeme vinapata hitaji hilo muhimu, kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa na kijamii.

Rais Samia azindua Shule 302 zilizojengwa na Boost, Sequip
Mkutano FAO wamfikisha Waziri Mkuu Italy