Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema upatikanaji wa Umeme Vijijini unaimarisha ubora wa elimu kwa shule za Msingi na Sekondari nchini na kwamba nia ya Serikali ni kuhakikisha mazingira ya ufundishaji na ya kusomea kwa watoto yanaimarishwa, ili kupata Viongozi bora wa kesho..

Kapinga ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuwasha umeme kwa mara ya kwanza katika Kijiji cha Ukata wilayani Mbinga wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Usambazaji wa umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa pili Mkoani Ruvuma.

Amesema “lengo la Serikali ni kuhakikisha tunaboresha mazingira ya ufundishaji ili walimu waweze kutumia vitendea kazi vinavyoendana na ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia, haiwezekani mwalimu asiwe na Kompyuta wala na Printer akiwa anafundisha ili kusaidia mtoto tutakuwa tunalea taifa la aina gani? Kwahiyo ni lazima kuweka umeme sababu Dunia nzima inaenda na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Kapinga amewaeleza Wananchi kuwa, maendeleo ni hatua hivyo mradi wa REA unatekelezwa kwa awamu katika vijiji vyote nchini, na ifikapo Desemba 2023 vijiji vyote vitaunganishwa na umeme na kama kuna kitakachosalia kitaunganishwa wakati wa kuunganisha vijiji 2024.

Tanzania kufanya mageuzi kiuchumi - Rais Samia
Rais Museven aishukuru Tanzania, ampa ujumbe Dkt. Biteko