Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inaendelea kutunga Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu na Mkakati wake wa utekelezaji kwa lengo la kuweka mfumo jumuishi wa usimamizi na uendelezaji wa rasilimali zake, ili kukuza uchumi wa nchi na maendeleo endelevu.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Abdallah Hassan Mitawi wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Uchumi wa Buluu na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Wizara za kisekta leo Oktoba 17, 2023 jijini Dodoma.

Amesema Uchumi wa Buluu ni dhana ambayo inachagiza ukuaji wa uchumi kupitia matumizi endelevu ya rasilimali maji kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira na ushirikishwaji wa jamii.

Bw. Mitawi mafunzo hayo yatawajengea uwezo washiriki kuhusu jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia programu ya Msaada wa Kibajeti pamoja na Kukuza na kuongeza ujuzi katika masuala ya uchumi wa buluu na mabadiliko ya tabianchi.

“Sote tunatambua kwamba mabadiliko ya tabianchi yapo na ni ya kweli na tayari athari zake zimeshaanza kuonekana na zimeleta madhara makubwa katika maeneo ya bahari na mito nchini kama tunavyoshuhudia vimbunga, El- Nino pamoja na kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari na mito,” amesema Mitawi.

Hivyo, kwa muktadha huo ametoa wito wa kuchukua kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kulinda na kuhifadhi Misitu yetu, vyanzo vya maji na rasilimali zote ambazo ndio tegemeo katika nyanja ya Uchumi wa Buluu.

Kwa mara ya kwanza Putin yupo China tangu aivamie Ukraine
Dereva ana haki kujua mwendokasi aliokamatwa nao - Polisi