Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza ziara ya Kitaifa ya siku tatu nchini Zambia kuanzia Oktoba 23 hadi Oktoba 25, mwaka huu ikiwa na lengo la kujenga ushirikiano kati ya nchi hizo mbili zenye historia kubwa kiushirikiano.

Katika ziara yake nchini humo, Rais Dkt. Samia pia amekubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Nchi ya Zambia, yatakayofanyika Oktoba 24, 2023, jijini Lusaka.

Mbele ya Waandishi wa Habari, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba, amesema maeneo ya kipaumbele katika ziara hiyo ni pamoja na namna bora ya kuboresha miundombinu inayounganisha Tanzania na Zambia ili kufikia faida za kiuchumi.

Aidha, ziara hiyo pia inategemewa kuangazia namna bora ya kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Zambia pamoja na kuibua fursa mpya za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwa kuzingatia Zambia ni lango la bidha zinazotoka Tanzania kwenda Zimbabwe na Kongo.

Cristiano Jr kutimiza ndoto zake Saudi Arabia
TP Mazembe, Simba SC kudumisha ushirikiano