Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema kuwa malengo yao ni kuhakikisha wanasonga mbele ingawa anaamini ataenda kukutana na upinzani mkubwa kutoka wapinzani wao Al Ahly ambao watakuwa nyumbani leo Jumanne (Oktoba 24).

Huu unakuwa mchezo wa nane kuzikutanisha timu hizi mbili kwenye mashindano tofauti michezo sita ya Ligi ya Mabingwa kila timu imeshinda mara tatu kwenye uwanja wake wa nyumbani huku mchezo wa saba ukiwa wa Ligi ya Soka Afrika (AFL) ulioisha kwa sare ya 2-2.

Akizungumza mjini Cairo, Misri Kocha Robertinho amesema kuwa kikosi chake kiko tayari kwa ajili ya mchezo huo ambapo anaenda kukutana na timu bora wanaheshimu hilo lakini lengo lao ni kutinga hatua ya Nusu Fainali.

“Nafahamu tutakuwa na mechi ngumu leo dhidi ya timu kubwa Afrika, ila kuna namna ambavyo tutaingia na mpango tofauti na ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza nyumbani.

“Tunawaheshimu Al Ahly ni timu kubwa yenye mashabiki wengi, lakini zimebaki dakika 90 ambazo zitaamua nani anasonga mbele. Nimewaambia vijana wangu wasahau matokeo yaliyopita akili na nguvu wahamishie kwenye mchezo wa leo,” amesema Robertinho

Amesema atakuwa na mabadiliko ya wachezaji kwenye baadhi ya maeneo ili kufanikiwa kucheza vizuri zaidi na kupata ushindi ili waweze kusonga hatua inayofuata.

Marcel Koller: Tunafahamu umuhimu wa mchezo huu
Washauri mikataba TPA na DP World iwekwe wazi