Serikali Nchini imeshauriwa kuweka wazi mikataba mitatu ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari – TPA na DP World, unaotarajiwa kuongeza ufanisi katika uendeshaji na utoaji huduma na kuongeza ajira kwa Watanzania, ili kuhakikisha kama maoni ya Wananchi yamefanyiwa kazi.

Ushauri huo, umetolewa kwa nyakati tofauti na Watanzania ambao wamesema wana mashaka na mikataba hiyo wakidai baadhi ya vipengele vilivyofichika vitaweza kuleta athari baadaye, hivyo Serikali iweke wazi ili kuwaruhusu Wananchi kuthibitisha kama maoni yao yamesikilizwa.

Mmoja wa Wananchi hao, Wakili Boniface Mwabukusi amesema Serikali uwekaji wazi wa mikataba iliyosainiwa utawezesha mjadala wa kitaalamu na kutoa fursa ya kufahamu kile walichokuwa wakikilalamikia katika mkataba wa utangulizina kwamba hawapingi uweekezaji huo unaotarajiwa kuongeza makusanyo ya kodi, ushuru wa forodha, na tozo mbalimbali.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jukwaa la Sauti ya Watanzania Dkt. Wilbroad Peter Slaa amesema hawakubaliani na mikataba hiyo iliyosainiwa na wataendelea na maandamano yasiyo na kikomo, ili kuishinikiza ifutwe kwani hakuna Serikali inayofanya kazi bila kufuata taratibu.

Wakati wa utiaji saini mikataba hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alisisitiza kuwa mkataba huo utalinufaisha Taifa na kuchangia katika maendeleo ya nchi na kwamba hakuna Mtanzania atakayepoteza ajira yake Bandarini.

Robertinho: Tutakuwa na mchezo mgumu Misri
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 24, 2023