Washambuliaji wanaoshukiwa kuwa ni Wanamgambo wenye misimamo mikali ya Kiislamu, wamewaua watu 26 kwa kutumia Mapanga usiku wa kuamkia Oktoba 24, 2023 katika mji wa Oicha, uliopo mashariki mwa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC.

Shambulio hilo, limethibitishwa na msemaji wa Jeshi la Kongo, Antony Mwalushayi pamoja na Meya wa Oicha ambao kwa pamoja wanalituhumu kundi la Wanamgambo wa ADF kuhusika na mauaji hayo ya kikatili kwa watu wasio na hatia.

Hata hivyo, Mwalushayi amesema shambulizi hilo dhidi ya raia, linaaminika kuwa la kulipiza kisasi dhidi ya mashambulizi ya hivi karibuni ya Jeshi ambayo yaliwalenga na kuwafurusha waasi.

Aidha, aliwaambia Waandishi Habari kwamba Wanamgambo walitumia panga badala ya Bunduki, ili vikosi vilivyoko karibu visiweze kusikia milio ya risasi.

Rais Dkt. Samia, Hakainde kuondoa vikwazo vya Biashara
Twiga Stars kuikabili Botswana Chamazi