Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatamani Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Julius Nyerere – JNHPP uanze mapema, ili Watanzania wapate umeme wa uhakika.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameyasema hayo wakati alifanya kikao na ujumbe wa Waziri wa Nyumba, Nishati na Maendeleo ya Makazi kutoka nchini Misri, Dkt. Assem Elgazzar kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa JNHPP jijini Dar es Salaam.
Amesema , Rais Samia ana matarajio makubwa kuhusu kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo na anatamani mwanzoni mwa mwaka 2024 utekelezaji wake uanze na kuongeza kuwa mradi wa JNHPP ndio mwarobaini wa kutatua changamoto ya hali ya upatikanaji wa umeme nchini.
Aidha, Dkt. Biteko ameishukuru Serikali ya nchi hiyo kwa kuonyesha ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo kwa wakati na kusisitiza kuwa, Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano ili mradi huo ukamilike kwa wakati.