Serikali za Tanzania na Zambia, zimesaini mikataba nane ya ushirikiano katika maeneo tofauti, kufuatia ziara ya kitaifa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Zambia.
Mikataba hiyo, ilifuatia mazungumzo ya ana kwa ana yaliyofanywa baina ya Rais Samia na mwenzake wa Zambia, Hakainde Hichilema kwenye Ikulu ya Zambia.
Maeneo muhimu katika makubaliano hayo yanahusu masuala ya ushirikiano baina ya nchi hizo kwenye biashara na Uwekezaji, Gesi Asilia, Ulinzi na Usalama, Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
Katika ziara hiyo, Rais Dkt. Samia na Rais Hichilema pia wameazimia kuweka mazingira yatakayofanya biashara kati ya Tanzania na Zambia kutokuwa na vikwazo.