Kocha Ange Postecoglou alikasirishwa na kiwango cha Tottenham Hotspur licha ya kuwalaza Fulham kwa mabao 2-0 na kuwa kileleni mwa msimanmo wa Ligi Kuu England, juzi Jumatatu (Oktoba 23).

Heung-Min Son na James Maddison walifunga mabao hayo na kuwapeleka Spurs pointi mbili mbele ya Manchester City na Arsenal, kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Lakini Postecoglou hakufurahishwa na uchezaji wa timu yake kwa ujumla.

Aliiambia Sky Sports: “Yalikuwa matokeo mazuri. Fulham ni timu ngumu, lakini tuliisimamia vema katika kipindi cha kwanza.

“Nadhani kwa nafasi tulizopata labda tungepata bao la pili na la tatu.

“Kipindi cha pili hakikuwa kizuri kwetu, hatukucheza popote karibu na viwango tulivyoweza, ulikuwa wakati wetu mbaya zaidi wa kumiliki mpira kwa msimu huu.

“Bila mpira bado tulikuwa bora. Bado tuna kazi kubwa ya kufanya.

“Siku zote unatakiwa kuheshimu mchezo. Nimekuwapo kwa muda mrefu vya kutosha kujua kama umejizuia kidogo, inaweza kukuangusha haraka sana.

“Hatukukaa sawa kwa mtindo wa soka, tunaotaka kucheza na tulichukua uhuru na mchezo ambao sikufurahishwa nao.

Ushindi huo umemhakikishia Postecoglou kuvunja rekodi ya kushinda pointi 23 kama kocha mpya ndani ya Spurs baada ya michezo tisa. Lakini Muaustralia huyo alikuwa na nia ya kutozingatia hatua hiyo binafsi.

Aliongeza: “Sichukulii hesabu, si baada ya kipindi cha pili. Kuna kazi nyingi ya kufanya.

Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 26, 2023
Tanzania, Zambia zasaini mikataba nane ya ushirikiano