Wahispania 200,000 wamekiri kudhulumiwa kingono na padri wa Kanisa Katoliki wakati walipokuwa wadogo, kufuatia Watu 8,000 walihojiwa na tume ya haki za binaadamu iiyoundwa nchini Uhispania, kuchunguza visa hivyo.

Katika uchunguzi huo, iligundulika kuwa karibu asilimia 0.6 ya watu wazima kwenye Taifa hilo la watu milioni 39, walidhulumiwa kingono na Mapadri hao, huku Kaimu Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez akisema kutolewa kwa ripoti hiyo ni hatua muhimu katika historia ya kidemokrasia ya nchi hiyo.

Ripoti hiyo yenye kurasa 777, pia inajumuisha matamshi ya wahanga 487 waliosema wanakabiliwa na changamoto za kihisia, zilizosababishwa na mikasa hiyo.

Aidha, ripoti hiyo imetoa wito kwa Serikali kuandaa fungu la kuwasaidia wahanga hao ambao asilimia 65 miongoni mwao, wakiaminika kuwa ni wanaume.

TAMWA-ZNZ yaendeleza kampeni haki za Watoto wa Kike
Jose Mourinho atafuta mlango wa kutokea