Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Justine Masejo amesema wanawashikilia wanafunzi wawili wa Chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (CDTI), kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanafunzi wa chuo hicho kwa njia ya mtandao.

ACP Masejo, ametoa taarifa hiyo hii leo Januari 29, 2023, na kuwataja waliokamtwa kuwa ni Efron Isaya (32) na Cosmas Robert (26), wote wanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo hicho.

Amesema, Januari 21 mwaka huu saa 11 jioni katika Chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (CDTI),  Wilaya ya Arumeru kuliripotiwa tukio la unyanyasaji wa kijinsia mwanafunzi wa chuo hicho,  (jina limehifadhiwa) kwa njia ya mtandao na wanafunzi wenzake.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Justine Masejo.

ACP Masejo amefafanua kuwa, baada ya kupata taarifa hiyo jeshi hilo lilianza uchunguzi wa tukio hilo na kufanikiwa kuwakamata wanafunzi hao wawili.

Amesema Polisi bado inaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mara utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Basi lawaka moto na kuuwa 41, watoto 10 wafa maji
Ukosefu wa tiba HIV, Ukimwi wasababisha vifo maelfu ya Watoto